TAASISI YETU YA VOICE OF CHANGE



Taasisi yetu ya Voice Of Change (V.O.C) ni muungano wa watu shupavu na imara kutoka pande zote za Tanzania wakiwa wahitimu wa fani mbalimbali kutoka vyuo vikuu, wanafunzi, wafanyakazi, wakulima,wafugaji ,na wenye kutoka katika sekta mbalimbali wenye  mzigo wa  kuinua jamii kupitia vipaji vyao.Taasisi hii ya Sauti ya mabadiliko ni taasisi ya kijamii, isiyo ya kisiasa,isiyo ya kiserikali,isiyo ya kidini,isiyo ya kidhehebu au ya kibiashara inayojikita katika shughuli mbalimbali za kuisaidia jamii kupata maarifa ya kibinadamu na kiutu ambayo inakusanya watu wenye mzigo na nia ya kuleta mabadiliko kwa njia ya kupata elimu, ujuzi na maarifa yanayohusu masuala mbalimbali ya kimwili,kitamaduni,kimaadili, kisaikolojia, kijamii, kiuchumi na kiroho na hatimaye kuelimisha watu wengine kuleta mabadiliko katika familia zao,maofisini,katika jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla .Taasisi hii pia inalenga kuamsha vipaji ,vipawa ,uwezo na karama za watu kwa njia ya kuwafanya wajitambue wenyewe ,wagundue hazina walizonazo ambazo hawatumii na baadaye kuwaelekeza namna ya kuzitumia katika kusababisha kuleta maabadiliko na maendeleo katika maisha yao na jamii inayowazunguka.

No comments:

Post a Comment