VOICE OF CHANGE TANZANIA ( V.O.C )
      Blog:voctanzania.blogspot.com
                                         
                                                          
TOPIC: KIJANA NA MABADILIKO
A.UELEWA JUU YA UJANA NA KIJANA: 
 Ujana ni hatua ambayo mtu anaipitia baadaya utoto au ni kipindi cha kati cha makuzi ya mtu kabla ya utu uzima na hatimae uzee. 
Ujana huanza mara baada ya mtu kubadilika kimaubile na huanzia miaka  kumi na mbili wengine hadi kumi na tano ambapo mtu huanza kuwa na hisia za kimwili na kutamani sana kuwa na uhuru wake katika maamuzi. 
Mabadiliko haya huchochea au hupelekea hisia mbalimbali za kimwili na mabadiliko ya jumla ya tabia 
Ujana ni majira yanayopita katika makuzi ya mwanadu, ukifanikiwa kuwa mzee ni lazima ulipita katika kipindi hiki au daraja hili la ujana, kwa hiyo kama bado uko katika dara hili ni muhimu kujipanga ili usije ukajilaumu mbele ya safari 
B.MABADILIKO NI NINI HASA?
Mabadiliko ni hali ya kutoka mahali Fulani kwenda sehemu nyingine,ni kuhama kutoka mahali ulipo kwenda mahali kwingine.
C.AINA MBILI YA MABADILIKO 
Mabadiliko yenye tija ka jamii(Mabadiliko mazuri)
Mabadiliko yasiyo na tija kwa jamii(Mabadiliko mabaya)
AINA YA MABADILIKO TUNAYOLENGA KATIKA VOICE OF CHANGE NI AINA YA KWANZA:
 Yaani mabadiliko ya:

Kisaikolojia
Kiuchumi
Kiutendaji
Kielimu
Kimwili (Afya )
Kimaadili
Kimtazamo
Kitabia
Kimaendeleo

D.DONDOO MUHIMU KUHUSU MABADILIKO
Mabadiliko yanaanza na wewe mwenyewe na sisi ndio wakala wa kusababisha mabadiliko.Mabadiliko huletwa na watu waliokusudia. .Mabadiliko yanaandaliwa hayatokei tu,yanaandaliwa,yanasababishwa na yanaundwa kwa mchakato mrefu sana.
Mabadiliko ya kweli hutokea baada ya watu kushirikiana pamoja ,kunia mammoja,kusheya mawazo,kusheya rasilimali zao,kujengana,kuhimizana,kutiana moyo,kukubaliana nk…
Mabadiliko ya kiuchumi hayawezi kutokea bila kuelimishwa (kushiriki semina za ujasiriamali ),au bila ya kujifunza kwa wajasiriamali walifanikiwa .nk…Si kila mabadiliko yana umuhimu katika maisha ya mwanadamu.
Tunapojifunza kutumia siri ya maombi,sala au dua  tunaweza kusababisha mabadiliko. Mungu habadilishwi na maombi,dua au sala bali maombi yanatubadilisha sisi na mazingira tuliyomo 
Mabadiliko ni kuamua kuachana na itikadi zote za kidini ,kikabila,kirangi,kisiasa,kidhehebu na kusonga mbele na jamii bila ya ubaguzi
E.VYANZO VYA MABADILIKO MAZURI NA YA KWELI:
1. Mungu(ALLAH) Mwenyewe
2. Mtu mwenyewe(Mindset yake) anapokubali kubadilika.
3. Kutumia rasilimali alizonazo mtu (dormant potentials)
4. Elimu (pasipo kuelimisha jamii ,ujinga hauwezi kumtoka mtu)
F.HATUA ZA KUFUATA KUFIKIA MABADILIKO YA KWELI
  
A.HATUA YA KWANZA NI KUJITAMBUA(SELF-AWARENESS)
Kujitambua ni hatua muhimu sana katika katika safari ya mabadiliko
Usifuate mkumbo jitambue kwanza kwa kujiuliza maswali yafuatayo:
a) Mimi ni nani?
b) Nimezaliwa au Nimeumbwa na Mungu kwa makusudi gani?
c) Nina nini?
d) Ninatoka wapi na ninaelekea wapi?
KIPIMO CHA KUJITAMBUA NI U.MA.FU.TI
a) UWEZO
Ni pamoja na Afya yako,Elimu,Wanafamilia,Uchumi uliyonao,Vipaji,Marafiki wazuri uliyonao…..
b) MAPUNGUFU
Tabia mbaya uliyonayo ,Ukosefu wa kuwa mbunifu,kushindwa kufanya maamuzi sahihi,kukurupuka,kutokupenda ushirikiano na wengine ….
c) FURSA
Mahali ulipo,Rasilimali watu waliokuzunguka ,Vipaji ulivyo navyo,Mungu 
d) TISHIO 
Ushindani kila kona mfano katika mahusiano,elimu,ajira,biashara,
Ibilisi mwenyewe hapendi ufanikiwe.Maadui zako ni wengi .Kwa hiyo usijisahau kumbuka kwamba mungu ndiye chanzo cha kila jambo jema hata maadui wakikujia Mungu akiwa upande wako hawawezi kufanikiwa hata kidogo.Basi mtangulize yeye kwa kwenda msikitini au kanisani bila ya kuvutwa na mtu yeyote. “Nje ya Mungu hakuna mafanikio yenye faida .”

UTAIJUAJE NAFASI YAKO KAMA KIJANA: 
Nafasi yako kama Kijana ni wajibu wako, umuhimu ulionao kwako na kwa jamii kwa ujumla wake pamoja na familia yako. 

LAZIMA UJUE NAFASI YAKO KATIKA MAENEO YAFUATAYO: 
• Kwako binafsi, • Kwa familia yako, • Kwa msikiti au kanisa lako, • Kwa jamii yako • kwa mkoa wako, • kwa taifa lako na Kwa Mungu mwenyewe. 

Safari ya kujua Nafasi yako katika maeneo yako hayo yote inaanzia katika neno moja tu: KUJITAMBUA. 
Jenga Ufahamu Hapa 
1. Kujitambua ni hatua ya muhimu katika maisha ya mtu yoyote duniani kama anataka kuishi kwa Furaha na matumaini na kufikia malengo yake 
2. Kujitambua ni matokeo ya kupata ufahamu sahihi juu eneo fulani utakaokusaidia kufanya maamuzi sahihi katika eneo husika ili uweze kufanikiwa 
3. Ufahamu au maarifa unapatikana kwa kutafuta, kuchunguza na kudadisi taarifa mbalimbali kwani si kila namna ya kujitambua ni sahihi kwa kijana 
4. Matokeo ya ufahamu ulionao yatafanana na ubora wa maisha unayoishi kwa kiwango cha kuathiri maamuzi yako ya kila siku 
5. Kiwango cha matokeo ya kujitambua kitafanana na ubora wa taarifa ulizozipata 
6. Udhihirisho wa maisha ya kujitambau ni hatua ya juu kabisa ya kuthibitisha kwamba kweli umejitambua 

KUJITAMBUA NI NINI?
 “Kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na nguvu ya taarifa unazopata” 
a. Ulishawahi kujiuliza ulizaliwa kwa kusudi gani?
b. Ujana ni zawadi kutoka kwa Mungu.
c. Mungu anajua umuhimu wa Kijana na Ibilisi anajua umuhimu wake pia.
d. Ili kuleta mafanikio na matokeo ya haraka Kijana ana uwezo mkubwa sana.
e. Ujana ni silaha nyepesi mno na hatari sana.

UMUHIMU WA KIJANA KATIKA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA:

1. Kutatua matatizo ndani ya jamii 
2. Kurudisha matumaini 
3. Kurekebisha hali ya mambo 
4. Kurudisha heshima iliyopotea katika jamii.
5. Kuwa mkarimu nyumbani
6. Kujitolea kifedha,Kiakili ,Muda 
7. Taifa lenye nguvu ni lile Vijana wao wanajitambua.
8. Kijana akikosa mwelekeo anaharibu mwelekeo mzima wa familia yake na taifa .
9. Vijana wachache tu wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana 
10. Kijana aliyebadilika moyoni mmoja tu anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana
11. Kijana asipojitambua na kuwajibika atadharauliwa tu kama hakuna kitu umekifanya katika familia yako kinachoonekana.
12. Una ulichokifanya katika jamii ya kwenu?
13. Penda kijana ukiwepo mahali uwepo kwa faida, usiwe hasara bali uwe faida.

B.HATUA YA PILI NI KUPANGA (PLAN)
Kuwa na maono au ndoto  
Kuwa na mikakati ya kutoka hapo ulipo
Kutafuta malighafi za kuondoa kiu yako (Look for resources that will enable your dreams to become true)
Kujikubali mwenyewe na Kujiamini kwamba unaweza (I CAN,I MUST,I WILL)
Kuondoa hofu ya kufeli

 C.HATUA YA TATU KUANDAA MTANDAO WA WATU(PEOPLE)
Hatua hii ni pamoja na kuomba ushauri,kuchangishana mawazo
Kushirikiana na watu sahihi(right people)
Kuachana na marafiki wabaya
AINA NNE ZA MARAFIKI:
1. RAFIKI WA KWELI
Ni yule rafiki:
anayekujali,anakujulia hali,anakutia moyo,mwenye nia ya dhati ya kukusaidia.
ukiumia anahuzunika,ukifeli anafadhaika,ukifurahi naye anashangilia.Anapenda kuona mafanikio yako.Anakuonya kwa hekima ,anakutetea na kukufariji.Hapendi kukuona ukiwa umenuna.Anakuombea,anakusaidia na anakukumbuka kwa njia mbalimbali za mawasiliano nk...Ana upendo wa agape kwako.

2. RAFIKI MNAFIKI
Ni yule rafiki:
asiye na upendo na wewe hata kidogo lakini anajidai kukupenda sana ingawa sivyo ilivyo.
Ukiwa naye anakusifia ,kukuinjoi kwamba anakupenda sana na hawezi kuishi bila wewe na maneno mengine mengi ya kinafiki .Anakuhoji maswali mengi ili apate maneno ya kwenda kukusema vibaya kwa wengine,kukusengenya na kukuteta vibaya.

3. RAFIKI MPOTEZA MUDA
Ni yule rafiki:
anayekudanganya kwamba muko pamoja lakini kiukweli yeye ana agenda ya siri usiyoijua.
Anakupotezea tu muda na kukuzehesha ,anakupotezea muda na kukupa stress.Na hatimaye baada ya muda fulani anatafuta sababu kama kisingizio cha kuvunja urafiki wenu kumbe alikuwa anajua tangu zamani.
4. RAFIKI MNYONYAJI
Ni yule rafiki 
anayejileta karibu na wewe kwa kulenga faida fulani  kwako maalum .Ana misheni maalum kwa ajili yako na anatumia mbinu zote zile kuhakikisha amekunasa ufahamu ili umtimizie kile anachokitana na baada ya kufanikisha basi ghafla anakuacha njia panda,anakuacha mwenyewe.
Faida hizo zinaweza kuwa : Fedha,Mwili wako,Ajira, Biashara  na mambo mengine mengi. 

D.HATUA YA NNE NI KUWA NA USTAHIMILIVU NA MSIMAMO KATIKA MAAMUZI ULIYOCHUKUA (PERSEVERANCE AND STAMINA)

E.HATUA YA TANO NI KUANZA MCHAKATO(PROCESS)
Anza kuchukua hatua ya kufanyia kazi mpango (uliyojiwekea wa kuitumikia jamii)

USHAURI KUHUSU MABADILIKO

Tukubaliane kuleta maendeleo sote kwa pamoja bila kuzingatia tofauti zetu za kidini, kiitikadi na hata kimtazamo na hakika kwa mantiki hiyo kila kitu kinawezekana,maana hakuna mtu asiye na kipaji sote tuna vipaji tofauti na sote tuna ndoto ya maisha mazuri.
Sijui kama kweli tunataka mabadiliko au tunaombea mabadiliko yatokee. 
Sijui kama tunafanya ili kusababisha mabadiliko au tunasubiri wengine wafanye ili tufurahie mabadiliko; 
Sijui hata kama tunajua vizuri ni mabadiliko gani hasa tunayataka na kama tunataka ni juhudi gani tumezifanya kushiriki kwenye mchakato wa kuleta mabadiliko hayo.
Tunaweza kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kujaribu kubadilishana mawazo mchana kutwa na usiku kucha lakini mabadiliko hayaji kwa kusema. Mabadiliko hayaji kwa kupigiwa magoti au kwa kukemea giza usiku. Mabadiliko husababishwa na kutekelezwa.Kubwa kuliko yote ili tuendelee inatupasa tubadilishe fikra zetu tusifikiri kushindwa, kwa namna yoyote ile ukifikiri kushindwa unashindwa. Sisi tufikiri kushinda tutashinda, tutekenye bongo tusilaumu, tutafute ufumbuzi wa maana tupende tulicho nacho tukione ni tunu. Ah! sijui nisemeje lakini yaani tukiwa na nia moja, tutafanikiwa.

Ni muhimu kila Kijana akafahamu mambo yafuatayo kuhusu yeye: 
1. Ni lazima ujitambue, upate ufahamu sahihi juu ya maisha yako pamoja na mambo yote na jamii inayokuzunguka 
2. Ni muhimu ujue wajibu ulionao kwako wewe mwenyewe kama mtu binafsi juu ya maisha yako 
3. Kuna haja ya kujua kuwa wewe ni sehemu ya familia yako na lazima ujue wajibu wako kwa wazazi na familia kwa ujumla 
4. Ni lazima ujifunze kuwa mzalendo wa taifa lako sawa na jinsi ambavyo Mungu anataka, fahamu kuwa umeunganishwa na ardhi ya Tanzania kwa mafanikio yako, Mungu akikwambia nenda nje ya nchi nenda lakini
 usifikiri mafanikio hayako Tanzania 
5. Kijana anatakiwa ajitambue, ajielewe yeye ni nani na ana kusudi gani katika maisha yake 
6. Unatakiwa kupata uelewa wa kutosha juu ya kipindi cha ujana na umuhimu wake ukiwa bado Kijana ili ujue namna ya kuzingatia na kujipanga kwa hapo baadae 
7. Kuelewa changamoto zilizopo katika kipindi cha ujana na namna ya kuzishinda kuna uhusiano na namna unavyojitambua ukiwa bado kijana 
8. Kujenga shauku, nia na kiu kwa kijana ili aweze kuishi maisha yenye mwelekeo na aweze kutimiza maono yake akiwasaidia na wengine kumjua Mungu na maisha yake kwa ujumla wake 
9. Kuwekeza uthamani na nguvu ya kipindi cha ujana kwa mtazamo wa Ufalme wa Mungu 



No comments:

Post a Comment